Jirani kalazimishwa
Kashikwa kinywa kwa fosi kapanuliwa
Pilipili kali katiliwa
Meza usiteme! Kashurutishwa
Hii ni halua meza, kimasomaso kahadaiwa
Mbona nisile nikitakacho? Auliza jirani
Kwa nini nile uamuacho? Aemewa
Jirani alia, taabani kajipata
Machozi yamtiririka ja maji mferejini
